Friday, August 19, 2011

PARAPANDA ILIVYOPAGAWISHA SWEDEN

Shabo akilicharaza gitaa wakati Parapanda ikiwasha moto jukwaani mbele ya mamia ya watazamaji nchini Sweden
 Bibie Eva Nyambe wa kikundi cha Parapanda Theatre Lab akipagawisha mashabiki nchini Sweden ambapo kundi hilo linafanya maonyesho yake
 Baadhi ya wasanii wa kundi mahiri la sanaa nchini Tanzania, Parapanda Theatre Lab, wakiwa jukwaani Sweden tayari kwa kuonyesha igizo la ANTIGONE ambapo kwa mara ya kwanza litaigizwa kwa lugha ya Kiswahili.
 Msanii Frank Samatwa(aliyeshika zeze) akionyesha umahiri wake katika kupiga zeze la kigogo wakati Parapanda ilipoonyesha igizo la ANTIGONE nchini Sweden. Pembeni yake ni Eva Nyambe na Amani Lukuli.

"Hata waTanzania tunaweza kupiga Djembe"-Daudi, msanii wa Parapanda akionyesha ufundi wake na ubunifu katika kuipiga ngoma ya Djembe yenye asili ya Afrika Magharibi wakati wa ziara yao nchini Sweden. Nyuma yake ni Shabo akimsindikiza kwa ngoma.

No comments: